Matthew 12:1-6

Bwana Wa Sabato

(Marko 2:23-28; Luka 6:1-5)

1 aWakati huo Isa alipitia kwenye mashamba ya nafaka siku ya Sabato. Wanafunzi wake walikuwa na njaa, nao wakaanza kuvunja masuke ya nafaka na kuyala. 2 bLakini Mafarisayo walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato.”

3 cIsa akawajibu, “Je, hamjasoma alichofanya Daudi na wenzake walipokuwa na njaa? 4 dAliingia katika nyumba ya Mungu, akala mikate iliyowekwa wakfu, yeye na wenzake, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya, isipokuwa makuhani peke yao. 5 eAu hamjasoma katika Torati kwamba siku ya Sabato makuhani huvunja sheria ya Sabato Hekaluni lakini hawahesabiwi kuwa na hatia? 6 fNawaambia wazi kwamba, yeye aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa.
Copyright information for SwhKC